DKT. TIZEBA ATOA MAFUNZO YA KUMSAIDIA MTOTO MCHANGA KUPUMUA

Posted on: April 17th, 2024


Na SRRH

Daktari Bingwa wa Watoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Shinyanga (SRRH), Dkt. Yustina Tizeba, leo Aprili 17, 2024 ametoa mafunzo ya kumsaidia mtoto mchanga kupumua (Neonatal Resuscitation).

Mafunzo hayo ameyatoa kupitia mwendelezo wa Elimu ya Vipindi vya Afya (CME), ambacho hufanyika kila Jumatano ya wiki katika Ukumbi wa Mikutano Hospitalini.

Akitoa somo hilo, Dkt. Tizeba amebainisha watoto wachanga wanahitaji uangalizi mkubwa na makini ili kuokoa maisha yao.

Halikadhalika ameongeza kuwa, mafunzo hayo yamelenga zaidi kukumbushana, kwa madhumuni ya kujengeana uwezo kwa watumishi wote wa afya.

Halikadhalika, Tizeba ameomba elimu aliyoitoa ikatumike vizuri kwa maslahi ya ustawi uzuri wa maendeleo ya watoto, huku akiwataka watumishi kushiriki mafunzo hayo pindi yanapofanyika ili kukuza uelewa.